Tulipokuwa Zimbabwe mwezi wa December tulikuwa tunaongea na baadhi ya wajumbe, tukawaza tuwe na pre-league games, tukamwita kocha Sven tukamuuliza mwezi January tutafanyaje maana kutakuwa na mapumziko marefu kupisha michuano ya CHAN 2020. Sven akasema tutafute mechi za kirafiki.”
Kabla ya kwenda Mapinduzi Cup Zanzibar nikamuuliza Sven kama yupo tayari nialike timu kwa ajili ya mechi za kirafiki, akakubali akasema kama timu zitatoka nje tualike moja kama za ndani nialike timu mbili.
Tulipokuwa Zanzibar tulikuwa tunapata kifungua kinywa tukawa tunajadili tutafanyaje ili kupata mechi za kirafiki ili kuendelea kuwafanya wachezaji wawe na match fitness wakati wa mapumziko ya CHAN, ndipo likaja wazo wa Simba Super Cup badala ya mechi za kirafiki za kawaida tu. Kwa hiyo Simba Super Cup ilizaliwa Zanzibar.
0 Maoni