Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Mambo 10 Simba Vs Al Hilal

Mambo 10  Simba vs Al Hilal




1: SIMBA SUPER CUP imezinduliwa Kikubwa, Kibingwa, Kibabe. Bila shaka salamu za Mnyama zimefika vizuri kule Sudan na vitongoji vyake

2: Kipindi cha kwanza, Simba walikwenda kuwaonyesha Al Hilal sanaa ya kumiliki mpira na Al Hilal walikwenda kuwaonyesha Simba sanaa ya kujilinda bila mpira. It's 4-2-2-2 vs 4-5-1.. Mzani ukabalansi

3: Kipindi cha Pili, Simba wakaswitch kwenye 4-1-2-3, Namba ikawa kubwa kwenye lango la Al Hilal.. Kasi ikaongezeka, Wakafunguka kwa Kuufungua uwanja. Wasudan wakapigwa na kitu kizito utosini

4: Inaonekana Falsafa ya kocha mpya wa Simba ni kushambulia kwa pasi fupi hadi kwenye eneo la mwisho la mpinzani. Akifanikiwa kuisuka vyema combination ya viungo wake watatu wa juu kwenye kumalizia shambulizi (Iwe kwa pasi au shuti) Wanaweza kutikisa zaidi

5: 'Plan B' ya Falsafa ya Da Rosa ilikuwa kwa Ben Morrison WHAT A PLAYER Ni katika siku kubwa, amelikumbusha Jiji Kubwa, Ukubwa wa Kipaji chake Aliwapa Simba kasi, ubunifu na Finishing nzuri kwenye eneo la mwisho

6: Bao la Al Hilal ni matokeo ya Poor organaization kwenye safu ya ulinzi ya Simba. Ni mara ya kwanza Simba kucheza na 'Back 6' ile. Ungetegemea kuona makosa ya aina ile pindi unapokutana na 'quality' kama ya Al Hilal

7: RALLY BWALYA Left Footer Magician Yuko katika muendelezo bora wa kipaji chake. Mguu wake wa kushoto ni hatari kwenye kuutunza/kuutuma/kuukimbiza mpira. What A Player




8: Taddeo Lwanga.. Yes he is Good kwenye Build Up. Ana faida kubwa Simba ikiwa na mpira, lakini bado anahitaji kuusukuma zaidi mwili wake kwenye kuutafuta mpira. Kwenye mechi zenye 'high Intensity' anaweza kuteseka sana

9: Al Hilal hawakumkaba Chama kwa man Marking.. Walimkaba kwa nafasi. Waliweka idadi kubwa ya watu kwenye zone ya 14 ya kiwanja hali iliyompunguzia nafasi/muda wa Chama kufikiria akiwa na mpira. Kuna somo makocha wetu wanaweza kujifunza pale

10: Kagere hakuwa na siku nzuri kazini. Chikwende pia aliteseka kuelewana na wenzake.. Mwisho, Mugalu anatakiwa kupunguza uchoyo

AMEANDIKA: Ally Kamwe

Chapisha Maoni

0 Maoni