Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram na Facebook Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba alisema
"Ndugu zangu wana-Simba. Napenda kuwataarifu kwamba sisi katika uongozi wa Simba tumejizatiti na kuweka mikakati ya kuhakikisha tunachukua tena Ubingwa wa Ligi, kuchukua Kombe la FA, na kufika mbali kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
Pia tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba Klabu yetu inajenga chapa na sifa bora Afrika na kote duniani. Sehemu ya mkakati huo ni haya mashindano tuliyoandaa ya Simba Super Cup, ambayo hadi sasa yamefanikiwa na yamepokelewa vizuri kote Afrika. Nia yetu ni kwamba mashindano haya ya Simba Super Cup tuyafanye kila mwaka. Tayari tumeanza maandalizi ya mashindano haya kwa msimu ujao ambapo tutaongeza idadi ya timu kubwa za Afrika. Nia yetu pia ni kwamba mashindano haya yajiendeshe yenyewe kibiashara. Vyanzo vya fedha za kugharamia mashindano haya ni:- wadhamini, malipo ya utangazaji, viingilio na mchango wangu binafsi.
Wito wangu maalum kwenu ni kwamba, ili mashindano yajayo yawe bora zaidi, nawaomba tuje uwanjani, tujaze uwanja kwenye mechi za haya mashindano. Tukija kwa wingi tutakuwa tumefanikiwa mambo manne:- tumechangia klabu yetu kimapato, tumeyapa mashindano haya hadhi na heshima stahili, tumevutia timu nyingine kubwa Afrika ziombe kuja kushiriki, na tumewapa wachezaji wetu moyo na hamasa.
Kwahiyo, nawaomba shime tuje uwanjani kwa wingi kwenye mechi yetu na TP Mazembe siku ya Jumapili, tarehe 31.01.2021. Pamoja na kwamba tunaweza kuitazama mechi kwenye luninga lakini mapato yatakuja Simba, na tutaweza kufanya mambo makubwa zaidi, kama tutakuja mpirani. Tuonyeshe mapenzi na uzalendo kwa Klabu yetu kwa kuja kwenye mechi. Hii pia itatupa moyo sisi viongozi kuendelea kubuni na kutekeleza mambo makubwa na mazuri zaidi. Shime, tukutane kwa Mkapa Jumapili saa kumi alasiri. Tuma huu ujumbe kwa mwana-Simba mwenzako.
Mohammed Dewji
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,
Simba Sports Club
30/01/2021 "
Alimaliza kwa kuandika hivyo pia licha ya ujumbe huh wengi wameonekana kusambaza katika ilikuungana naye
0 Maoni