Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Mambo 10 Mchezo Kati ya Simba Sc na TP Mazembe

Mambo 10 nilioyaona Simba vs TP Mazembe




1: SHOO YA KIBABE. SHOO YA KIKUBWA. Mechi yenye hadhi kubwa. Mechi yenye ubora mkubwa. Tactically, Technically Mashabiki wamenjoy mpira wa viwango vikubwa

2: Jeuri ya Simba mbele ya Mazembe kiufundi ilisababishwa na Class ya baadhi ya wachezaji wao katikati ya kiwanja. Mazembe walipogundua ni hatari kuruhusu One v One kati ya Chama na Koffi, wakarudi chini kucheza kwa Tahadhari. Simba wakanufaika kuutanua uwanja na kushambulia kwa tempo kubwa

3: TP Mazembe wana wachezaji bora wanaoweza kuibeba Timu pindi mpango wa mwalimu unapofeli. Hiki ndio kitu Simba wanachotakiwa kujifunza kutoka kwao. Kipa wao, Beki wao kati, Kabasso Chongo na kiungo Koffi walikuwa na ubora binafsi ulioipa suluhu Mazembe

4: Luis Miquissone Definitely huyu ndiye mchezaji hatari zaidi kwenye kikosi cha Simba. Alikuwa bora kwenye kumkimbiza Ochaya, akawa bora kwenye kukaba akiidhibiti kasi ya Isack Tshibangu! Ni ndoto ya kila kocha kufanya kazi na mchezaji wa aina hii

5: Chris Kisangala .. What A Player Yule kiungo wa TP Mazembe mwenye breach kichwani.. Ana kila kitu cha mchezaji mzuri. Kimo, Kasi, ufundi na akili ya kusoma mpira Mguu wake wa kushoto ulikuwa na maswali mengi kwa Lwanga

6: Joash Onyango STOPPER ya Viwango Alicheza dhidi ya mastraika wakubwa na yeye akawaonyesha ukubwa wake kwenye kukaba. Timing yake kwenye mipira ya juu ilikuwa superb sana

7: Kameta 'Duchu' .. Somehow amepata mechi za kumpa kipimo cha wapi anatakiwa kujiboresha zaidi. Hakufanya vibaya lakini bado ana mengi ya kujifunza katika safari yake

8: Bwalya na Morrison wamerejesha heshima yao kikubwa kwenye mechi kubwa. Ni wajibu wao kulinda viwango vyao ili kumpa kocha 'Option' nyingi kwenye hatua ya makundi

9: Lwanga amecheza vyema lakini kiungo wa chini wa Mazembe Koffi Kouame ni kioo chake cha kujitazama. Lwanga ana ubongo wa kusoma njia za mpira na kuzuia lakini hana mamlaka kwenye eneo lile.  Simba inamuhitaji upesi arejee kwenye 'Fitness' yake

10: Asante Mohammed Hussein Kipindi cha kwanza alikomaa na Isack Tshibangu, Kipindi cha pili akaletewa 'kijeba' Bibonge Lakini akamudu kukimbizana nacho


AMEANDIKA: ALLY KAMWE

Chapisha Maoni

0 Maoni