Mechi Dume, mechi ya Kiume iliyochezwa na Wanaume.
Heko kwa Mbwana Makata na Kongole kwa Didier Gomes.
Kuna nyakati timu inaweza kupoteza mchezo kisha ukasawajika Nafsi kutokana na namna ambavyo wachezaji wamewajibika.
Katika makala yangu ya mwisho kuandika nilisema kuwa timu nyingi zinazokaa nyuma ya Mpira huwa zinafeli katika matendo ya Pili.
Pale ambapo wanaunasa Mpira huwa wanakosa makali wanapokwenda kushambulia na hupoteza Posession ndani ya dakika chache.
Leo Dodoma walikuwa bora sana wakati wa kufanya safari na mawinga wao walikuwa wanapokea Mipira nyuma ya safu ya Ulinzi ya Simba.
Simba waliingia na mfumo wa 4-4-2 kwa maana walikuwa na kiungo mmoja tu wa Ukabaji ( Thadeo Lwanga ).
Timu yoyote Duniani ambayo inatumia kiungo mmoja wa ukabaji huwa kuna mashimo yanaachwa pale ambapo wanakwenda kushambulia.
Faida ya kuwa na viungo wa wawili wa chini ni pale ambapo wapinzani wanauchukua Mpira hawa viungo wawili wanautanua uwanja na kuziba mashimo.
Lwanga aliwekwa katika nyakati ngumu sana, ndio maana alishatepeta ndani ya dakika 60 tu kutokana na kazi kubwa aliyokuwa anaifanya.
Kila Mpira ambao Dodoma waliunasa walishambulia kupitia pembeni.
Unasifu ile sharpness ( Uharaka ) ya mawinga wao ambao muda wote walikimbia nyuma ya safu ya Ulinzi.
Kuna nyakati hata uwe mkubwa kiasi gani unapaswa kumuheshimu mdogo, heko yangu kwa Gomes iko hapa.
Alipotambua kuwa timu yake imepoteza uimara katikati na Plan ya kutumia Krosi haileti faida akabadilisha aina ya uchezaji.
Nyakati ambao Simba inashambulia ilikuwa na viungo washambuliaji watatu nyuma ya Meddie Kagere na wakawa wanatumia pasi mpenyezo kwenye eneo la mwisho.
Simba ikapata goli kwa aina hiyo na haraka akabadilika tena kwa kumuingiza Mzamiru ili acheze pacha na Lwanga.
Simba ikaongeza uimara katikati na Dodoma Jiji ikawa sio hatari kwenye kutengeneza mashambulizi kutokana na Mipira kuwa blocked (kuzuia)

IMEANDIKWA: SOKA PLACE
0 Maoni