BAADA ya kutokuwa hali si shwari ndani ya klabu ya Yanga, golikipa Metacha Mnata ameibuka na kuzua utata.
Mnata ambaye alidaka mechi ya Polisi Tanzania iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 ameandika maneno ambayo yamezua utata kwenye mitandao ya kijamii.
Metacha ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram;" Nawashukuru kwa wote na pia kwa kunipa sapoti katika miaka miwili na nilifurahia maisha yangu nikiwa Yanga nawatakia kila la kheri katika mafanikio yenu,".
0 Maoni