Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA na Prison Mchezo wa Kibabe Leo

Simba inapambana na Prisons leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa lakini rekodi za kibabe zinawabeba Wekundu wa Msimbazi.




Mara nyingi timu hizo zinapokutana jijini Dar es Salaam, Simba imekuwa ikipata ushindi kirahisi ingawa leo kocha msaidizi wa Prisons, Shaban Kazumba ameapa kukomesha uteja kwa wapinzani wao.

Rekodi zinaonyesha katika michezo nane iliyopita iliyopigwa Dar tangu 2012, Prisons imepoteza saba huku mchezo mmoja tu timu hizo zikitoka suluhu.

Prisons pia ilishawahi kukutana na kipigo kikubwa kutoka kwa Simba cha mabao 5-0 Februari 28, 2015.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mgumu kwani Prisons haiko sehemu salama kwenye msimamo wa ligi hivyo inahitaji kushinda ili kujiweka sehemu nzuri kwenye ligi ili kujiepusha na janga la kushuka daraja.

Simba yenye pointi 45 katika nafasi ya pili kwenye msimamo inafukuzia kupunguza pengo la pointi kati yake na vinara Yanga wenye pointi 50 huku Wanajagwani wakisheza mechi nne zaidi.
Wekundu wa Msimbazi wana hasira ya kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Oktoba 22 mwaka jana kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.

“Tumejipanga kushinda mechi hii,” alisema kocha Kazumba wa Prisons yenye pointi 27 nafasi ya 10.

Chapisha Maoni

0 Maoni